Jumatatu 20 Oktoba 2025 - 07:44
Wafanyakazi na Wanafunzi Nchini Hispania wafanya Mgomo kwa ajili ya kuwakingia kifua Wapalestina

Hawza/ Wafanyakazi na wanafunzi wa Hispania walifanya maandamano makubwa ya kuiunga mkono Palestina tarehe 15 Oktoba, ambapo takriban maelfu ya watu walishiriki kutoka sehemu mbalimbali za Hispania.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, watu pia waliikosoa serikali ya Pedro Sánchez kwa kutochukua hatua za kimkakati za kuwapiga marufuku Waisraeli, licha ya kutangaza rasmi lawama kwa mauaji ya kimbari (genocide) huko Ghaza.

Hatua hizi nchini Hispania zilifanyika masaa machache tu baada ya mfululizo wa maandamano na migomo miwili ya kitaifa nchini Italia, ambayo pia yalilenga mahitaji sawa ya kumaliza vitendo vya Israel na kuonyesha mshikamano na Palestina. Watu wanaamini kwamba nyakati hizi ni muhimu kwa ajili ya harakati za kijamii barani Ulaya.

Coral Latorre, kutoka umoja wa wanafunzi, katika moja ya maandamano alifanya mahojiano na kusisitiza jukumu muhimu la wanafunzi na vijana katika kudumisha mshikamano na Palestina. Alifafanua kuwa takriban wanafunzi 25000 walishiriki katika maandamano ya Madrid, na maelfu zaidi walijihusisha na maandamano huko Barcelona, Tarragona, Valencia na miji mingine mwanzoni mwa mwezi huu.

Latorre alisema: "Leo sisi wanafunzi hatuko tu katika mgomo, bali jamii ya wafanyakazi pia ipo pamoja nasi." Kuanzia alfajiri, kugoma, kuziba njia, mikusanyiko katika kampuni na viwanda ilianza kutekelezwa. Tulisema kwamba tutafunga kila kitu, na hii ndiyo siku hiyo — kama mtaendelea kutuma silaha na rasilimali kwa Israel, na Israel kwa ushirikiano wenu watakata meli za misaada ya kibinadamu, tutaingia tena mitaani.

Kuchanganyikiwa na kukata tamaa kutokana na sifa za maneno tu juu ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotangazwa hivi karibuni na Rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wa Israeli, kulichochea maandamano hayo. Waandamanaji waliukosoa kwa uchungu uongozi wa viongozi wa Ulaya kwa kutoa lawama lakini kuendelea kuuza silaha na vitu vya kijeshi kwa Israel.

Chanzo: Peoples Dispatch

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha